Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Balozi wa Marekani nchini, Dk, Donad Wright amesema kwasasa kuna sera zinazoifanya Zanzibar na Tanzania kuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutoka nchini kwake.
Dk. Wright ambaye yupo nchini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, aliyasema hayo juzi wakati akizindua ofisi ya Dar es Salaam ya kampuni ya uuzaji na ukodishaji wa majengo ya Re/Max ambayo asili ni Marekani.
Amesema tangu alipoteuliwa kuiwakilisha nchi yake hapa nchini, kipaumbele chake kimekuwa ni kukuza urari wa biashara baina ya Tanzania na Marekani na mwaka huu nchi hizo zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano.
“Hivi karibuni nilifarijika kusikia Serikali ya Zanzibar na imetangaza mpango unaowaruhusu wawekezaji wa kigeni kuchukua fursa za unafuu wa kodi na vibali vya makazi visiwani humo.
“Sera za namna hiyo zinaendelea kuifanya Tanzania na Zanzibar kuwa kivutio zaidi cha wawekezaji wa Kimarekani,” amesema Balozi huyo.
Upande wake, Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Jamal Kassim ambaye alikuwa sehemu ya walioshuudi ufunguzi wa ofisi hiyo amesema hivi aribuni Zanzibar imepitisha sera ambayo ni kivutio kikubwa cha uwekezaji katika sekta ya makazi visiwani humo.