27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru Musoma yawataka watumishi wa umma kuzingatia maadili

Na Shomari Binda, Musoma

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mara,imewataka watumishi wa Umma kuzingatia maadili katika utumishi wao.

Akizungumza leo Julai Mosi 2021 mjini Musoma Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Takukuru, Amosi Ndege, amesema maadili ni nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Amesema wananchi wanawategemea sana watumishi wa umma katika kuwahudumia kwenye maeneo mbalimbali hivyo ni muhimu kuwa na maadili.

Ndege amesema mtumishi anapokosa maadili ni vigumu kutenda haki wakati wa kutoa huduma kwa yule mwenye uhitaji, na kuongeza kuwa maadili yanabeba vitu vingi ikiwemo uadilifu na pale mtumishi akikosa uadilifu atajiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

“Tunasisitiza sana suala la maadili kwa watumishi wa umma kwa kuwa ndio nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa. Mtumishi anapozingatia maadili hawezi kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na makosa,” amesema Ndege.

Kwa upande wake Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara, Hassan Mosi, amesema wataendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwenye maeneo mbalimbali. Amesema elimu ni jambo muhimu ili kumfanya kila mmoja kuwa balozi katika mapambano dhidi ya Rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles