Goma, Kongo
Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, limetoa ripoti ya kuwaokoa watoto 530 waliopotea baada ya kutenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha yao wakati wa mlipuko wa Volkano.
Mlipuko huo wa Volkano uliotokea siku ya Jumamosi Mai 22, 2021 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku karibu nyumba 500 ziliharibiwa baada ya Mlima Nyiragongo, ambao uko sehemu ya Kaskazini mwa mji wa Goma, kulipuka.
Afisa wa Unicef mjini Goma, Jean Metenier alisema wamefanikisha kuwapata karibu watoto 530 ambao walitenganishwa na wazazi wao na kufikia sasa tumewakutanisha Watoto 360 na wazazi wao,
Pia ameongezea na kusema kulikuwa na hali ya wasiwasi juu ya mlipuko ulipotokea usiku wa Jumamosi na karibu watu 25,000 walilazimika kuondoka maeneo yaliyoathirika zaidi.