23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, October 16, 2021

Zaidi ya Watoto 500 wapatikana Kongo

Goma, Kongo

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, limetoa ripoti ya kuwaokoa watoto 530 waliopotea baada ya kutenganishwa na wazazi wao walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha yao wakati wa mlipuko wa Volkano.

Mlipuko huo wa Volkano uliotokea siku ya Jumamosi Mai 22, 2021 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku karibu nyumba 500 ziliharibiwa baada ya Mlima Nyiragongo, ambao uko sehemu ya Kaskazini mwa mji wa Goma, kulipuka.

Afisa wa Unicef mjini Goma, Jean Metenier alisema wamefanikisha  kuwapata karibu watoto 530 ambao walitenganishwa na wazazi wao na kufikia sasa tumewakutanisha Watoto 360 na wazazi wao,

Pia ameongezea na kusema kulikuwa na hali ya wasiwasi juu ya mlipuko ulipotokea usiku wa Jumamosi na karibu watu 25,000 walilazimika kuondoka maeneo yaliyoathirika zaidi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,801FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles