29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wajasiriamali Kiliamanjaro wahamasishwa kujiunga na NSSF

Na Safina Sarwatt,Kilimanjaro

Wajasriamali wadogo Mkoa wa Kilimanjaro wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF), ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo ikiwemo mikopo na kuweza kuboresha biashara zao wanazozifanya.

Ushauri huo umetolewa na jana na Afisa Matekelezo ya Wanachama wa hiari kutoka NSSF Mkoa wa Kilimanjaro Hussein Kaku, wakati akizungumza kwenye kongamano la Chama cha Wafanyabiashara mkoa wa Kilimanjaro (TWCCC), lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwashirikisha wajasiriamali zaidi ya 150.

Amesema wajasiriamali hao baada ya kujiunga na NSSF wataweza kunufaika na mikopo ya kibiashara ambayo itawasaidia kuwasaidia kukuza biashara zao.

Kaku amesema wajasiriamali hao wataweza pia kunufaika na aina mbali mbali za mafao yanayotolewa na mfuko huo ikiwemo fao la uzazi pamoja na fao la kustaafu kama ilivyo kwa wachangiaji waliopo katika mfumo rasmi.

“Niwaombe wajasiriamali mkoa wa Kilimanjaro, kuchangamkia fursa hii, baada ya NSSF kuruhusu wajasiriamali kujiunga na uanachama,” amesema.

Aidha, ameongeza kusema kuwa “Fursa nyingine zinazopatikana kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja na Sh milioni 8 hadi milioni 50 zinazotolewa na NSSF kwa wazalishaji wadogo na kwamba fedha hizo urejeshaji wake ni ndani ya miaka 7 ambapo kwa miezi sita itakuwa ni bure,”amesema.

Alifafanua kwamba fursa nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja na pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, Mafao ya uzazi na mafao ya kuumia kazini.

Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa wa Kilimanjaro, Large Materu, alisema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuwawezesha makundi ya wanawake na vijana walioko katika vikundi vinavyojihusisha na shughuli za ujasiriamali ambavyo vinatambulika kisheria .

Nao baadhi ya wajasiriamali walioshiriki kongamano hilo Teddy Komba, na Jamila Bakari, wamesema kuwa fursa ya wao kuruhusiwa na NSSF kujiunga katika mfuko huo utawainua kiuchumi kwa kuwa licha ya kunufaika na mafaoa ya NSSF lakini pia wataweza kupata mikopo kupitia hisa zao ambazo zitawainua kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles