22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

TFS wananchi wanalojukumu la kuendelea kutunza mazingira

Na Safina Sarwatt, Moshi

Wananchi wanaozunguka Hifadhi za Misitu Asilia zilizopo chini ya TFS, wanalo jukumu la kuhakikisha kwamba kila mmoja anaendelea kutunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa bayonuai zilizopo katika misitu hiyo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwemo binadamu.

Wito huo umetolea Mei 2,2021 na Afisa Misitu Msaidizi, Solomon Meisila, wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kuitembelea Hifadhi ya Msitu Asilia wa Rau, uliopo Mjini Moshi.

Meisila amesema misitu imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani, ikiwepo kuwa na makazi ya wadudu, wanyama, ndege na eneo sahihi la kujipatia chakula.

Amesema ikolojia ya Msitu Asilia wa Rau imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa upatikaji wa chemichemiza nyingi za maji ambayo yamekuwa yakitumika kunyeshea mashamba ya mpunga yaliyopo maeneo ya Mabogini na Pasua.

“Kukiwa na miti mingi utapata hewa safi, ajira, mvua, chakula, matunda rutuba kwenye udongo na utapata mazingira ya kuishi,”amesema Meisila.

Amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti ya asili ovyo ili kuepuka kuharibu Mazingira kwa makusudi nankuleta madhara makubwa katika maisha ya binadamu na wanyama.

Aidha Afisa Misitu huyo Msaidizi amesema TFS, imeendelea kutoa elimu shirikishi kwa wananchi wanaozunguka Msitu Asilia wa Rau kwa kufanya mikutano mbali mbali ikiwemo vikao kwa lengo la kuwataka kuendelea kuyatunza mazingira.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Msitu Asilia wa Rau Godson Ollomi, amesema kutokana na uhaba wa maeneo baadhi ya wakazi wanaozunguka hifadhi hiyo wamekuwa wakivamia mara kwa mipaka ya hifadhi hali ambayo imekuwa ikiathiri shughuli za utunzaji wa Msitu huo.

“Msitu huu unazungukwa na Mitaa sita hivyo kumekuwepo na uvamizi wa mipaka ya mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likiathiri Sana shughuli zabutunzaji wa msitu huu,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles