Na Brighiter Masaki
-Dar es Salaam.
Kamanda Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, amewataka Polisi kuimarisha ulinzi Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa watani wa jadi timu ya wekundu wa msimbazi Simba na Young African Yanga.
Akizungumza na waandishi wa habari, mapema leo, Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa watani wa jadi.
“Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaochezwa uwanja wa Mkapa tarehe Mei 08, 20kujitokeza. majira ya saa 11 jioni.”
“Tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.”amesema Kamanda Mambosasa
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto uwanjani kuwaangalia kwa karibu au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kujitokeza
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka kufika uwanjani mapema ili kuepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani hapo kwani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha.
Pia tunawataka mashabiki kushangilia kwa amani na utulivu wawapo uwanjani ikiwa ni pamoja na kuepuka mambo yafuatayo
Mihemuko na maneno ya kuhasimiana kati yao.
“Kuingia na chupa za maji majukwaani
Kuingia na silaha ya aina yoyote
Kupaki magari ndani ya uwanja pasipokuwa na kibali maalum
Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziruhusu” amesema Kamanda Mambosasa