26.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za NTS na Bosch kunufaisha mafundi magari vijana Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya magari ya NasTyre Services Limited (NTS) ambayo ni waagizaji na wasambazaji wa matairi na betri imeongeza huduma zake nchini kupitia ushirika wa kibiashara ilioingia nao hivi karibuni na kampuni ya Bosch ambayo ni kampuni mashuhuri ya magari ya Ujerumani.

Pamoja na ushirikiano mpya, NTS imeongeza huduma zake kutoka kwa matairi na usambazaji wa betri hadi bidhaa na huduma zaidi za magari ikiwa ni pamoja na; usambazaji wa vipuri, kituo cha huduma ya dizeli na kuhudumia  magari kwa kutumia wataalamu wa Bosch.

Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess (wa pili kushoto)na Mkurugenzi wa Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS), Navin Kanabar wakitaka utepe kuzindua ushiriakiano wa kibiashara na utengezaji wa vifaa vya magari ya Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani, Dar es Salaam.

NTS imeeleza kuwa ushirikiano mpya na Bosch, kutafanikisha kutawala soko katika sekta ya utoaji huduma za magari nchini Tanzania.

Aidha, kutokana na ushirikiano huu, NTS inakuwa  kituo kinachowezesha mteja kupata huduma zote za magari yao katika sehemu moja.

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa NTS, Amin Lakhani akizungumzaleo Aprili 29, 2021 jijini Dae es Salaam amesema kuwa: “Tunajivunia kwa kuuza bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa sambamba na huduma bora, kwa kipindi cha miaka 10 sasa Watanzania wamekuwa wakinufaika na uwekezaji wetu katika sekta hii, kwa sababu hiyo, tumeona ili kukuza zaidi huduma zetu tutumie fursa hii kushirikiana na Bosch kibiashara ili kuendelea kuwapa wateja wetu huduma bora zaidi  na kwa gharama nafuu.

“Pamoja na kuongezwa kwa huduma za Bosch katika huduma zetu, mafundi magari wa Tanzania na vijana kwa jumla watapata fursa za mafunzo pamoja na mafunzo maalum nje ya nchi ili kukuza ujuzi wao, kwa maneno mengine, kupitia ushirika huu, NTS inafungua milango ya fursa kwa  vijana wa kitanzania katika sekta hii,” amebainisha Lakhani.

Mkurugenzi wa Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS),Navin Kanabar akizungumza baada ya kuzindua ushiriano wa kibiashara na Kampuni ya utengezaji wa vipuri bora vya magari ya kutoka nchini Ujerumani  ya Bosch, uliofanyika Dar es Salaam.

Akizungumzia ushirikiano wake na NTS, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Bosch, Dirk Appelt amesema NTS ina uhusiano mzuri katika tasnia ya magari na inajulikana kwa ubora wake, huduma za hali ya juu: “Kwa hivyo kutoka kwa mtazamo wa biashara, ushirikiano huu utanufaisha pande zote mbili,” amesema.

Mkurugenzi Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Utengenezaji wa vipuri vya Magari ya Bosch, Dirk Appelt (kushoto) akimkabiti tuzo ya ushiriano wa kibiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya ya NasTyre Services Limited (NTS), Navin Kanabar wakati wa uzinduzi,uliofanyika Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Kampuni ya ya NasTyre Services Limited (NTS), Amin Lakhani.

NTS ilianzishwa mnamo 1994 kama kiwanda kutengeneza upya matairi yaliyotumika, tangu wakati huo ilianza kuagiza na kusambaza matairi mapya na betri za magari  sehemu mbalimbali nchini kote ikiwa na vituo vya usambazaji katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.

Upande wake Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess amepongeza ushirikiano baina ya kampuni hizo mbili na kwamba itaendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani ambao umedumu kwa muda mrefu.

Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess(wa akiangalia mashine za kisasa za utengenezaji wa vipuri vya magari ya Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS)  baada ya kuzindua ushiriakiano wa kibiashara na utengezaji wa vifaa vya magari ya Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani, Dar es Salaam.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles