Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Moses Kaaya, amewataka Jeshi la Polisi (JKT) kukamilisha mradi wa Hospital iliyopo Kimara Baruti kwa haraka ili wananchi wawezekupata matibabu.
Akizungumza na www.mtazania.co.tz mapema leo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Manispaa ya Ubungo, Kaaya amewataka JKT kukamilisha mradi kwa wakati ili ianze kutoa huduma.
“Wananchi wa Kimara Baruti wanahitaji huduma ya matibabu ya haraka hivyo niwaombe, JKT kufanyakazi usiku na mchana ili kuweza kukamirisha mradi wa hospital kwa wakati.
“Lengo ni wanachi wapate huduma ya matibabu kwa haraka kwasababu walizoea kwenda mbali kupata matibabu lakini kwasasa utakapo kamilika watapata huduma zote,” amesema Kaaya
Kwa upande wake mkazi wa Kimara Baruti, Happiness Kileo, amesema kuwa mradi unaendelea vizuri na wanaipongeza serikali kwa maendeleo wanayowapelekea wananchi hasa ya matibabu.