Shirikisho la Soka nchini England (FA), limeitoza Chelsea faini ya pauni 65,000, wakati huo West Brom kwa ikipigwa faini ya pauni 35,000.
Mshambuliaji wa Chelsea ambaye anaonekana kuwa na utovu wa nidhamu, Diego Costa, alihusika katika mambo mengi yaliyoashiria kwamba ni ya utovu wa nidhamu.
Mhispania huyo alishambuliana na kiungo wa kati wa West Brom, Claudio Yacob, baada ya kuangushwa chini.
Katika mchezo huo, West Brom walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, ambapo klabu hiyo ilifanikiwa kutoka sare ya 2-2 dhidi ya wapinzani hao.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, FA inasema kuwa timu zote mbili zilishindwa kudhibiti wachezaji wake.
Hata hivyo, mchezaji ambaye alisukumana na Coasta, Yacob, alioneshwa kadi ya njano na kocha wake, Tony Pulis, aliamua kumtoa nje mchezaji huyo.
Siku chache baadaye kocha wa Chelsea, Guus Hiddink, alielezea kutoridhika na uamuzi wa refarii wa mchezo huo, Anthony Taylor, akisema kuwa alipaswa kumuonesha kadi nyekundu Yacob.