30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

DC awacharaza bakora wanafunzi kwa kuuza viti vya shule

Na Janeth Mushi, Arusha

-ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenan Kihongosi amewacharaza bakora, wafanyabiashara wanne wa vyuma chakavu pamoja na wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Sinoni, wakituhumiwa kufanya biashara ya viti vilivyotoka katika shule hiyo.

Wafanyabiashara hao wanadaiwa kununua viti hivyo kutoka kwa wanafunzi hao wanaotuhumiwa kuiba shuleni hapo. Kihongosi ametoa adhabu hiyo leo Desemba 16, shuleni hapo ambapo hadi sasa viti zaidi ya 108 vyenye thamani ya Sh milioni 10 vinadaiwa kuibiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Kenani Kihongosi akiwaadhibu kwa viboko wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya Sekondari Sinon waliokamatwa wakituhumiwa kuiba viti shuleni hapo na kuuza kama vyuma chakavu

Kihongosi amesema wafanyabiashara hao waliokamatwa na ushahidi wa viti hivyo wanaendelea kuwa rumande na kuhakikisha gharama za viti hivyo vilivyopotea wanalipa wakishirikiana na wazazi wa wanafunzi hao. 

Amesema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha watoto wanapata elimu lakini anasikitishwa kuona wafanyabiashara wakinunua miundombinu iliyopo shuleni hapo.

“Serikali inatoa fedha nyingi kuhakikisha elimu inaendelezwa ili taifa liondokane na ujinga leo mnanunua kiti kimoja Sh 500 wakati kiti hicho kinatengenezwa kwa gharama ya Sh 100,000 huu ni ujinga hamfikirii thamani ya miundombinu inayotolewa na serikali?,” amehoji Kihongozi.

Aidha, amemwagiza mkuu wa shule hiyo kuhakikisha watoto wanaodaiwa kuiba viti kusimamishwa masomo hadi wazazi watakapolipa viti hivyo.

Wazazi wa wanafunzi waliokamatwa wamekiri kuwa watoto wapo nyumbani baada ya kusimamishwa na uongozi wa shule hadi kikao cha bodi kitakapofanyika kwa ajili ya maamuzi juu ya watoto wao.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi akimcharaza kwa fimbo mmoja wa wafanyabiashara wa chuma chakavu anayedaiwa kununua viti hivyo

“Tumelipokea kwa masikitiko jambo hili la watoto wetu kuhusishwa na wizi wa viti kwa kuwa tunajitahidi kuhakikisha wanasoma, wakati mwingine tunalala hadi njaa kwa ajili yakutoa mahitaji yao lakini matokeo yake wanajiingiza kwenye makundi yasiyofaa,” amesema Saruni Laizer, mmoja wa wazazi watoto hao

Upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Nteles Lorna amesema hadi sasa wamebaini upotevu wa viti 108 baada ya kumalizika kwa mitihani ya kidato cha Nne.

Amesema wamebaini kupungua kwa viti  hivyo na walipoanza uchunguzi baadhi ya wanafunzi walianza kubainika kuhusika na wizi huo.

“Tulianza kuweka mitego hadi kwa walinzi na juzi ilipokuwa sikukuu ya Uhuru Desemba 9, mlinzi aliona watoto hao wakirusha viti juu ya ukuta na kuvichukulia nje ya ukuta na kuvipeleka kwa wauzaji wa vyuma chakavu,” ameema Lorna.

Operesheni ya kuhakiki miundombinu ya Shule hiyo ilifanywa na Afisa Tarafa ya Elerai iliyopo mkoani Arush, Titho Cholobi na baada ya kubaini upotevu huo alimshirikisha Mkuu wa Wilaya.

“Nilipata taarifa kwa wasamaria wema na nilifika kuona hali ilivyo na tulifanikiwa kuwatembelea wanunuzi waliohusika na kwa bahati nzuri wamekamatwa lakini tukawakamata na watoto 8 wanaohusishwa na jambo hili,”amesema

Nae, Diwani wa Kata ya Sinoni, Michael Kivuyo amesema kata hiyo  ina idadi kubwa ya wauzaji wa vyuma chakavu pamoja na watoto wanaoacha kwa makusudi kwenda shuleni na kujiingiza katika biashara hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles