27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

60 WAZALIWA MKESHA WA KRISMASI DAR

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WATOTO 60 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Kati ya idadi hiyo, watoto wakike ni 31 na wa kiume ni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana wilayani Ilala, Theresia Akida alisema katika mkesha huo watoto 28 walizaliwa.

“Kati yao wa kiume ni 16 na wa kike ni 12, waliozaliwa kwa njia ya upasuaji ni watatu, wa kike wawili na wa kiume ni mmoja, na wote wanaendelea vizuri” alisema Theresia.

Katika Hospitali ya Mwananyamala iliyoko Wilaya ya Kinondoni, jumla ya watoto 16 wamezaliwa kati ya watoto wanaume ni 8 na wanawake ni 8.

Ofisa Muuguzi kutoka Hospitali ya Mwananyamala, Zulfa Juma,  alisema mtoto mmoja ndiye aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji huku wengine wakizaliwa kwa njia ya kawaida.

Naye Mkunga Msaidizi daraja la tatu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amina Kadashari  alisema watoto tisa wamezaliwa katika mkesha huo hospitalini hapo.

Alisema kati ya watoto hao watano ni wa kiume na wa kike ni wanne ambao afya zao na mama zao zinaendelea vizuri.

Kwa upande wa Hospitali ya Temeke watoto waliozaliwa katika mkesha huo ni wanane ambapo kati yao wanawake ni saba na wa kiume ni mmoja.

Ofisa muuguzi wa zamu hospitalini hapo, Hamisa Shabani alisema kati ya watoto waliozaliwa wawili ni mapacha.

“Wote waliojifungua wanaendelea vizuri pamoja na watoto wao na mpaka sasa hatujapata changamoto yoyote ilitokana na hali hiyo wamelazimika kuishi maisha magumu na wengi kurudi sehemu walizotoka.

“Wapo walimu waliokuja na familia zao huku Butiama wao wameamua kubaki hapa hapa lakini wengine wamerudi sehemu
zao za kazi walikotoka kuendelea na maisha mengine wakati wanasubiri uhakiki wa wafanyakazi hewa utakapokamilika,”alisema mhadhiri huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles