30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

BALOZI LUSINDE AWAPA DARASA BODABODA

Balozi Job Lusinde
Balozi Job Lusinde

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

MWANASIASA mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde amewahadharisha vijana kutambua kuwa hatua ya kukosekana mfumo thabiti wa kusimamia huduma za bodaboda kuna hatari ya wao kushindwa kusimamia haki zao.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki mkoani hapa, wakati akifungua Umoja wa Waendesha Bodaboda Tanzania (TAMOSA), ambapo alisema yeye kama mlezi wa umoja huo ana wajibu wa kuhakikisha unakuwa imara na wenye manufaa kwa vijana wote nchini.

“Baada ya vijana hawa wa TAMOSA kufanya utafiti wa kina ilionekana umuhimu wa kuunda chombo hiki kama wenzetu madereva wa teksi na magari makubwa ya abiria na mizigo.

“Kukaa kwao kwa muda mrefu na kupitia malengo na katiba yao kwa makini niliona wanakuja na ajenda ya maana. Hata hivyo baadaye nikawaamini na kuwaunga mkono kwa malengo ya kusaidia sekta ya bodaboda kupunguza ajali,  kuongeza fursa ya ajira na kuimarisha huduma ya usafiri na kuboresha uchumi wa vijana na Taifa kwa ujumla,” alisema Balozi Lusinde.

Aliwataka vijana hao kujipanga kibiashara kwa kuhakikisha wanatoa fursa za ajira kwa vijana kupitia sekta hiyo ndogo ya usafirishaji.

“Natoa wito kwa kushirikiana na vyombo vya dola, bodi ya wadhamini itazame na kufikiria mambo ya msingi ya ujasiriamali, kupiga kelele vijana hawa wawe na bima ya afya, bima ya maisha na kuangalia faida za chama kwa kupigania haki za wanachama, kuwatambua na kutimiza wajibu wa kufuata sheria,” alisema.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Mwandamizi wa Mfuko wa Kuendeleza Hifadhi za Wanyamapori Barani Afrika (AWT), Pratik Patel alitoa ya kuhakikisha anawaunganisha vijana hao na kwa kuwa na taasisi imara yenye tija kwao.

Patel ambaye ni mwakilishi wa taasisi kadhaa za kimataifa za hifadhi ya mazingira ikiwemo World Conservation Fund na African Wildlife Trust anahusika na kampeni za kitaifa na kimataifa za kuendeleza utalii na kudhibiti ujangili dhidi ya tembo na kuendesha biashara  mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles