25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGZI CHADEMA WANUSURIKA KICHAPO

NA RAMADHANI LIBENANGA, MOROGORO

WANANCHI  na wagombea udiwani wa Chama  Cha  Demokrasia  na Maendeleo (Chadema)   katika  Kata nane  za Manispaa  ya Morogoro  wamevamia ofisi za  chama hicho wakitaka  ufafanuzi wa majina ya wagombea wa udiwani waliokatwa   wakiwa wameshinda katika  kura za maoni.

Ghasia  hizo  zilizuka  saa  9.00 mchana   baada  ya makundi  ya  wagombea  kutoka  katika  Kata  za Kionda, Kichangani, Kilakala, Lukobe, Mlimani, Boma, Mjimpya na Kiwanja  cha Ndege  kuvamia  ofisi  hiyo    kupata ufafanuzi wa  sababu za majina  yao  kukatwa  wakati wakiwa wameshinda  katika  kura za maoni.

Wanachama  walivamia  gari  la mwenyekiti wa  Chadema  wa wilaya  na kumzuia  asiondoke  hadi atakapotoa  ufafanuzi  wa madai hayo.

Mmoja  wa  wagombea   aliyekatwa  jina  lake  huku akiwa  ameongoza  katika mchakato wa  kura  za maoni, Mwanahenzi Shaha  alisema  ameshangazwa  na  hatua hiyo.

“Mimi  katika  Kata ya Mlimani  nimeshinda  kura za maoni lakini nashangaa leo naambiwa  jina langu hakuna na tayari ameteuliwa mtu mwingine hii ni rushwa,” alisema  huyo  kwa  hasira.

Mmmoja  wa  wanachama aliyekuwapo  katika  msafara huo  aliyejitambulisha  kwa  jina  la Fiderik Boniface,  alidai    kitendo  cha viongozi wa  wilaya  na mkoa  kukata baadhi ya   wagombea  kitaleta madhara  makubwa katika  chama.

Juhudi za kuwapata viongozi wa Chadema ngazi ya wilaya na mkoa  hazikuzaa matunda baada ya simu zao kutokuwa hewani   jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles