25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

TFDA yapiga marufuku aina 36 za vipodozi nchini

hiiti_b_silloESTHER MNYIKA NA MGENI SHABANI DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imezuia utengenezaji wa vipodozi tofauti 36 vya   krimu na losheni ambavyo vimebainika  kuwa na viambato vya steroids vilivyopigwa marufuku.

Vipodozi vilivyobainika kuwa na viambato  vilivyopigwa marufuku ni pamoja na siri moisturizing cream lemon, cocoa butter krimu,siri moisturizing  cream lemon,lovely body cream lemon, lovely body cream.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kwa matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vilivyovitengeneza.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alisema vipodozi hivyo vimetengenezwa na kampuni nne    nchini pamoja na Afrika Kusini.

Alivitaja viwanda vilivyozuiwa utengenezaji huo kuwa ni   Chemi & Cotex Limited vya Dar es Salaam ambavyo vimepigwa marufuku kuzalisha vipodozi sita huku Kiwanda cha Mamujee Product Limited cha Tanga kikizuiwa kutengeneza vipodozi 11.

Viwanda vingine ni Tanga Pharmaceutical & Plastic Limited ambacho kimezuiwa kutengeneza vipodozi 15,Tridea Cosmetics Limited cha Dar es Salaam (vipodozi 3) na Johnson & Johnson (pvt) Ltd, Rattray Road, East London,  (Afrika Kusini).

“Steroids iliyowekwa ndani ya vipodozi hivyo ni   dawa ambayo hutumika kutibu magonjwa ya ngozi ambayo mtu hutakiwa kutumia  ndani ya wiki mbili kwa kufuata ushauri wa daktari,”alisema Sillo.

Alisema baadhi ya madhara yanayosababishwa na dawa hizo ni   muwasho, kuvimba ngozi, ngozi kuwaka moto, ngozi kukatikatika na kupata chunusi kubwa kwenye ngozi.

“Mbali na kuwakataza kutengeneza pia tumefuta usajili wa vipodozi 31 vilivyokuwa tumevisajili    na kuwaelekeza mameneja wa ofisi za kanda kufanya ukaguzi wa maeneo yao kwa kushirikiana na ofisi za halmashauri  kuondoa sokoni vipodozi vyote vilivyohusika,”alisema Sillo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles