29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YATAKA MPANGO MPYA WA UCHUMI APEC

HANOI, VIETNAM

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amewaeleza viongozi wanaoshiriki katika mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki, APEC, kuwa Marekani imepata changamoto katika mikataba iliyopita.

Akizungumza katika mkutano huo, Trump aliulaumu utawala wa Marekani uliopita kwa kuruhusu hali hiyo kukua na kuendelea, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mataifa barani Asia, yakiongozwa na China, kuwa na nguvu zaidi katika soko huru la biashara na kuua soko la ajira nchini Marekani.

Trump ametolea mfano taifa la China na mengineyo kwa kuingia mikataba ya kibiashara inayolenga kuyanufaisha zaidi mataifa hayo na kuyawezesha kuuza zaidi bidhaa zake nchini Marekani kuliko yanavyoingiza bidhaa katika mataifa yao.

Ameongeza kuwa, kwa sasa anafikiria kuanzisha ushirikiano mpya wa kibiashara na mataifa ya nchi za Pasifiki kwa kuingia mikataba ya kibiashara na nchi ambazo zitakuwa tayari kuheshimu makubaliano ya mikataba hiyo kwa maslahi ya pande zote.

Trump ameueleza mkutano huo wa kilele kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki kuwa, sasa atahakikisha Marekani na nchi wanachama wa APEC wanakuwa washirika kibiashara kwa muda mrefu, huku pia akipongeza mafanikio ya kiuchumi yaliyokwishapatikana hadi sasa.

Aidha, Trump ametoa mwito kwa makampuni binafsi ya kibiashara kuwa na nafasi kubwa katika kujihusisha na mikataba hiyo ya kibiashara na kukosoa hatua ya serikali kuingilia zaidi masuala ya kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles