CHRISTOPHER MSEKENA
HAKUNA ambaye hajui kuwa mtaani kuna ngoma mpya inaitwa Bugana kutoka kwa nyota wa muziki hapa Bongo William Lyimo ‘Billnass’ na Faustina Charles ‘Nandy. Ni wimbo uliopokewa vyema, ndani ya muda mfupi umefanikiwa kukamata chati mbalimbali za muziki.
Katikati ya mafanikio hayo, Swaggaz tunakupa tatu safi na tatu chafu za wawili hawa, ambao wamekuwa gumzo wiki hii katika mitandao ya kijamii kutokana na ukaribu wao.
TUANZE NA SAFI
UMOJA WAO UNAWABEBA
Mara nyingi wanapokutana wanamuziki wapenzi au waliowahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wakafanya ngoma moja, mapokezi ya wimbo huo huwa ni makubwa kutokana na kila mmoja wao kumiliki mashabiki zake.
Kama ilivyowahi kutokea kwa Jux na Vanessa Mdee kupitia kolabo zao Juu na Sumaku, ndiyo hivyo hivyo ilivyotokea kwenye Bugana, wimbo wa Billnass aliomshirikisha Nandy, mrembo aliyewahi kuwa naye kwenye mapenzi na katika malavidavi yao wote wawili wanakiri kuwa walipendana japo walidumu kwa muda mfupi.
Billnas ana mashabiki wake hali kadharika Nandy pia ana wafuasi wake na wapo pia waliokuwa wanayashabikia mapenzi yao, hivyo wote hao wameungana kuubeba wimbo Bugana, kiasi kwamba ndani ya muda mfupi imekuwa ngoma kubwa.
WANAJUA KUCHEZA NA MASHABIKI
Moja ya bao walilofanikiwa kulifunga wawili hawa ni kujua namna ya kucheza na mashabiki zao. Wanafahamu kuwa wengi wana shauku ya kujua kama wamerudiana au laa maana ni kapo inayovutia machoni.
Hakuna anayejua kama wamerudiana au laa. Wao wenyewe wanajiita kaka na dada lakini matendo yao wanaoyanyesha katika mitandao ya kijamii yanaashiria wapo kwenye dimbwi zito la mahaba. Mkanganyiko huo unawaweka mashabiki kwenye mataa na kufanya waendelee kuwafuatilia.
NI VIJANA WAPAMBANAJI
Safi ya mwisho ya Billnas na Nandy ni vijana wapambanaji walioamua kutumia vipaji vyao kusaka mkate wa kila siku. Unaweza kuona Nandy mwenye miaka 26 sasa ameweza kufanya makubwa kwenye muziki ikiwamo kuanzisha tamasha lake mwenyewe na kuwaalika wasanii wengine akiwamo Billnas kutumbuiza.
Nayaona mafanikio makubwa zaidi mbeleni kwa Billnas, ambaye ndani ya muda mfupi ameweza kujitengenezea umaarufu, fedha na kuzalisha muziki mzuri ambao toka aanze kuachia wimbo wa kwanza Ligi Ndogo mpaka Bugana hajawahi kuchuja.
CHAFU ZAO
KUTUMIA HISTORIA YAO MBAYA
Mwaka uliopita ulikuwa mbaya kwa wawili hawa. Kama unafuatilia burudani bila shaka unakumbuka zile picha na video zenye ukakasi zikiwaonyesha Billnass na Nandy wakiwa katika mambo yao ya faragha.
Iliwapa matatizo makubwa, iliwachafua kweli kweli lakini Mungu akasaidia na kila kitu kikawa sawa. Kupitia historia hiyo mbaya tunaona wawili hawa wakiitumia kusukuma kiaina wimbo wao Bugana.
Ndani ya ngoma hiyo kuna mstari Nandy anaimba ‘Harafu mfukoni mambo mbaya. Hawatudai hata wavujishe picha mbaya’. Bila shaka picha mbaya zinazotajwa hapo ni zile zilizovujishwa mwaka jana.
KWANINI WATUMIE KIKI?
Binafsi nauamini sana uwezo wa Nandy na Billnass. Ni vijana wenye vipaji vikubwa ambavyo havihitaji kiki ili kusukuma ajenda zao. Ila katika kipindi hiki napata mashaka kwanini waitane kaka na dada wakati waliwahi kuwa wapenzi, hivi unaweza kumuita dada au kaka mpenzi wako wa zamani?
Wangeweza kuitana ‘Ex’ lakini hiyo isingewapa nafasi ya kujadiliwa kwa kiwango kikubwa, ndiyo maana wameamua kuitana dada na kaka ili iwe kama kiki ya kusindikiza ngoma yao.
CHIKUPIZI WAJIFUNZE NINI KWAO
Mtaani kuna marapa kibao wanatamani kuja kuwa kama Billnass hali kadharika kuna wasichana wengi wanatamani kuwa waimbaji mahiri kama Nandy. Sasa wawili hawa ambao wanatazamwa na chipukizi kama mfano leo wanatumia historia yao mbaya kuibua mjadala ili wapate nafasi ya kuzungumzwa siyo sawa. Wasanii wengi wachanga wanaweza kuhisi kuwa kiki za mtindo huo ni njia rahisi ya kutusua kisanaa kumbe si kweli bali ni jitihada, ubunifu na kujituma kwa Billnass na Nandy ndiyo kumewapa mafani