33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamke mwenye miaka 73 ajifungua mapacha, mumewe apata kiharusi hapo hapo

NEW DELHI, INDIA

MWANAMKE  mwenye umri wa miaka 73 katika jimbo la Kusini mwa India la Andhra Pradesh amejifungua watoto wawili mapacha wa kike.

Wazazi waliomsaidia kujifungua mapacha hao wanasema amejifungua kwa njia ya kuanguliwa kwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadae kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi ama IVF kwa lugha ya kitaalamu.

“Mama na watoto kwa pamoja wanaendelea vizuri,”Dk. Uma Sankar ameimbia BBC.

Mangayamma Yaramati amesema yeye na mumewe ambaye ana umri wa miaka 82, wamekuwa wakati wote wakitaka kuwa na watoto lakini hawakuwahi kupata mtoto hadi sasa.

“Tumefurahi sana ,”amesema mume wake, Sitarama Rajarao, akiongeza kuwa mkewe alipata ujauzito katika kipindi cha miezi miwili tu baada ya kufanyiwa matibabu ya IVF.

“Tulijaribu mara nyingi kupata watoto na tukawatembelea madaktari wengi ,” Alisema Yaramati  na kuongeza kuwa;

 “kwa hiyo hiki ni kipindi cha furaha zaidi maishani mwangu,”.

Aliongeza kuwa alihisi kutengwa na jamii na wanakijiji wenzake na mara kwa mara amekuwa akitengwa katika mikusanyiko kwasababu yeye hakuwa mama.

Anasema :”walikuwa wananiita mwanamke asiye na mtoto ,”

Lakini siku ambayo watoto wake mapacha walipozaliwa, mume wake Rajarao alipata kiharusi na kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini.

Mapacha hao wasichana walizaliwa kwa njia ya upasuaji, jambo ambalo ni la kawaida kwa uzazi huo wa nadra.

Mwaka 2016, mwanamke mwingine wa India aliyekuwa na miaka 70 , Daljinder Kaur, alijifungua mtoto wa kike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles