29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga ‘yawajadili’ mamluki wa Simba

_DSC0112NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Yanga ulikuwa na kikao kizito na wenyeviti wa matawi ya klabu hiyo, moja ya hoja iliyojadiliwa ni baadhi ya wachezaji wao kudaiwa kuwa ni mamluki wa watani zao Simba.

Kikao hicho kimefanyika siku chache mara baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 dhidi ya mtani wake, Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, huku baadhi ya wachezaji wakihusishwa kuihujumu timu yao na kupelekea kila mara kushindwa kuwafunga wekundu hao.

Baadhi ya wachezaji wanaotuhumiwa ni mabeki Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, viungo Haruna Niyonzima na Simon Msuva na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, ambao wanadaiwa kuwa na mapenzi na Simba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya timu hiyo Mtaa wa Jangwani, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alisema wameshauriwa na viongozi wa matawi kubadilisha mfumo wao wa usajili ili kuweza kuwafunga Simba kwenye mechi zijazo.

“Siwezi nikasema kuna mchezaji alihujumu timu, tulifungwa mabao rahisi tulipocheza na BDF XI kule Botswana, lakini mabao kama yale tukifungwa kwenye mechi ya Simba au Azam inakuwa tatizo, bao lile tulilofungwa lilikuwa la kimchezo na hakuna sababu ya hujuma. Ila kwenye kikao tulichokaa leo, viongozi wametushauri tubadilishe mfumo wetu wa usajili ili kuwa na njia sahihi ya kusajili wachezaji,” alisema.

Sanga alisema katika kikao hicho viongozi wa matawi wameomba wanachama wa timu hiyo na uongozi kwa ujumla kusahau yaliyopita ya kufungwa na Simba na kuunganisha nguvu kuelekea mchezo wao wa Jumapili hii dhidi ya Platinum, ikwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles