29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Azam ni mwendo wa visasi tu

azamNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

BAADA ya kulipa kisasi dhidi ya timu ya JKT Ruvu kwenye mchezo uliopita, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Azam FC wameapa kuendeleza wembe huo watakapoivaa Ndanda FC kesho.

Jumamosi iliyopita Azam iliifunga JKT bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex na kulipa kisasi cha kufungwa kama hivyo mzunguko wa kwanza.

Azam itaingia uwanjani kesho ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Ndanda bao 1-0, kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Kocha Mkuu wa muda wa Azam, George Nsimbe ‘Best’, aliliambia MTANZANIA jana kuwa, amekipanga kikosi chake kuibuka na ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Ndanda na kulipa kisasi cha mzunguko wa kwanza.

“Kama ilitufunga mzunguko wa kwanza Ndanda itakuwa ni timu nzuri, hivyo hakutakuwa na kitu kingine zaidi ya kulipa kisasi.”

“Lengo letu ni kushinda tena kama tulivyofanya kwenye mechi iliyopita, kwani malengo yetu makubwa ni kutetea ubingwa wetu,” alisema.

Nsimbe huenda kesho akamwanzisha mkongwe, Amri Kiemba kuchukua nafasi ya kiungo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ atakayekuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu.

Azam hivi sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 30 pungufu ya pointi moja dhidi ya Yanga anayeongoza ligi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles