23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

13 kizimbani kwa tuhuma za kuwaua watafiti Dom

pinguNa RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WATU 13, wakiwamo wanne wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi, Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini, wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watafiti watatu wa kituo cha Serian cha mkoani Arusha.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joseph Fovo na kusomewa mashtaka yao na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Beatrice Nsana.
Ndugu waliofikishwa mahakamani hapo ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Iringa Mvumi, Albert Chimanga, Cecilia Chimanga,  Julius Chimanga na David Chimanga.

Watuhumiwa wengine ni Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Msaulwa, Juma Madehe, Sostheness Mseche, Lazaro Kwanga, Yoram Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba.

Akisoma mashtaka hayo, mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa, washtakiwa waliwaua watafiti hao Oktoba mosi, mwaka huu, katika Kijiji cha Iringa Mvumi, wilayani Chamwino.

Aliwataja waliouawa kuwa ni aliyekuwa dereva, Nicas Magazine na watafiti wawili Teddy Lumanga na Jafari Mafuru.

Baada ya kusoma shtaka hilo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kutokana na hali hiyo, walirudishwa mahabusu hadi Oktoba 31 mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena.

Watafiti hao waliuawa Oktoba mosi na miili yao kuchomwa moto wakiwa kijijini hapo baada ya kudaiwa kuwa ni wanyonya damu.

Wakati wanauawa, watafiti hao walifika kijijini hapo kufanya utafiti wa udongo wakitumia gari lenye namba za usajili STJ 9570, aina ya Toyota Hilux, mali ya Kituo cha Utafiti cha Serian cha mkoani Arusha.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani hapa lilifanya operesheni maalum na kufanikiwa kuwatia mbaroni wananchi zaidi ya 30 waliokuwa wakidaiwa kuhusika na mauaji hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles