30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

100 waugua kipindupindu

kipindupinduNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

IDADI ya wagonjwa wa kipindupindu katika Mkoa wa Dar es Salaam imeongezeka kutoka 56 hadi 86.

Idara ya Kinga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pia ilisema jana kuwa, kuna wagonjwa 14 wa kipindupindu katika Mkoa wa Morogoro.

Mtaalamu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko katika idara hiyo, Elibariki Mwakapeje, alitoa takwimu hizo jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya siku moja kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo.

“Tunahitaji kushirikiana katika kukabiliana na ugonjwa huu kwa kuweka mazingira safi, maana unasambaa kwa kasi. Januari mosi mwaka huu ulianzia huko mkoani Kigoma, ukabainika Mwanza, Mara, sasa upo Dar es Salaam na Morogoro,” alisema Mwakapeje.

Alisema, hadi jana kulikuwa na wagonjwa 76 wilayani Kinondoni, watano katika Wilaya ya Temeke na sita Ilala.

“Kinondoni wagonjwa 18 wamewekwa katika uangalizi kwenye kambi maalumu ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu ili usizidi kusambaa,” alisema.

Kwa mujibu wa Mwakapeje, ili kukabiliana na ugonjwa huo, licha ya kutengwa kwa kambi hizo, pia Serikali imeandaa magari maalumu ya kubeba wagonjwa yatakayopuliziwa dawa.

“Jamii ikiona mtu anaugua ugonjwa wenye dalili za kipindupindu basi watoe taarifa mapema hatua zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na watendaji wa jiji waweze kufika na kupulizia dawa ili usizidi kusambaa na wajiepushe na mikusanyiko kama misibani maana ni hatari,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, amepiga marufuku uuzwaji wa matunda na vyakula katika mazingira hatarishi kuzuia mwanya kwa ugonjwa huo kuzidi kusambaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles