25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kumbaka mtoto wa miaka nane

AVELINE KITOMARY NA COSTANCIA MUTAHABA-DAR ES SALAAM 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam, imempandisha kizimbani Francis Mwakajila (25) kwa shtaka la kumbaka mtoto wa miaka nane.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha mashtaka wa Jamuhuri, Matarasa Hamisi, alidai Januari 14, mwaka huu eneo la Kimara B, Wilaya ya Ubungo, mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. 

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena. 

Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya milioni moja. Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakaposomwa tena Machi 18, mwaka huu.

  Wakati huo huo, watu watatu Yusuph Ibrahim (40), Cornelius Mohamed (26) na Goat Juma (49), wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha. 

Wakisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Veronika Mtafia, alidai Machi 28, mwaka jana eneo la Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa waliiba gari yenye namba za usajili T 943 CJY aina ya Suzuki Carry yenye thamani ya Sh 9,000,000 mali ya Leriver Athumani na kabla na baada ya kuiba, waliwatishia Oltetei Leseku na Saningo Molel kwa bastola ili kujipatia mali hiyo. 

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na kurudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya milioni moja. Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakaposomwa tena Machi 18, mwaka huu. 

Wakati huo huo, watu watatu Yusuph Ibrahim (40), Cornelius Mohamed (26) na Goat Juma (49), wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha. 

Wakisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Veronika Mtafia, alidai Machi 28, mwaka jana eneo la Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa waliiba gari yenye namba za usajili T 943 CJY aina ya Suzuki Carry yenye thamani ya Sh 9,000,000 mali ya Leriver Athumani na kabla na baada ya kuiba, waliwatishia Oltetei Leseku na Saningo Molel kwa bastola ili kujipatia mali hiyo. 

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na kurudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles