30.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Maambukizi VVU kwa mahabusu, magereza yatisha wadau

Ashura Kazinja – Morogoro

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, amesema mrundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani, kumetajwa kuchangia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hususani kwa wafungwa wanaume.

Takwimu zinaonyesha kuwa  kwa mwaka 2018, wafungwa na mahabusu  15,250 walipimwa na kati yao 340 walibainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo. Masauni alisema hayo wakati  wa ziara ya Kamati ya Bunge  ya Masuala ya Ukimwi ilipotembelea Gereza la Kingolwira  lililopo Manispaa ya Morogoro.

Alisema maambukizi ya Ukimwi gerezani limekuwa ni tatizo kubwa na jitihada za kupunguza tatizo hilo  ikiwemo kutoa elimu kwa wafungwa  na mahabusu na kupima kwa hiyari mara kwa mara zikitafutwa.

“Hali halisi ya maambukizi ya VVU kwa mwaka 2018 ni kwamba, jeshi la magereza lilipima wafungwa na mahabusu 15,250, wanaume wakiwa 13,961 na wanawake  13,334 na kati ya hao, 340 walikutwa na maambukizi, wanaume wakiwa 292 na wanawake 48 sawa na asilimia 2.2, huku wafungwa 1436 wakiwa wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU magerezani,” alisema Masauni.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo (CCM), Oscar Mukasa, alilishauri jeshi hilo kutoa taarifa  sahihi  na kutafuta ufumbuzi  wa changamoto hiyo na kwamba Watanzania wanaoishi na VVU ifikapo mwaka 2020 wawe wanajua hali zao.

Mkuu wa Tiba Magereza ambaye ni Kamishna  Msaidizi  Mwandamizi wa Magereza, Dk. Hassan Mkwicha, alisema si kweli kuwa watu huingia wazima magerezani na kutoka wakiwa si salama.

Alisema hupokea wafungwa na mahabusu toka sehemu mbalimbali, wengine wakiwa wagonjwa au na majeraha mbalimbali yakiwemo ya moto na kwamba wamekuwa walezi wazuri ambao hupelekea watu hao kutoka wakiwa salama.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles