25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dk Abbas aahidi kusaidia wanafunzi

Na JOHN KIMWERI (DSJ)DAR ES SALAAM

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas, ameziagiza taasisi za habari za umma kutoa nafasi za mafunzo kwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya sekta ya habari.

Dk Abbas aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 23 ya wahitimu wa kozi ya uandishi wa habari ngazi ya cheti na diploma katika Chuo cha uandishi wa habari cha Dar es Salaam (DSJ).

Alisema suala la mazoezi ya kuandika habari katika vyombo vya habari imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi na hivyo alizihimza taasisi kuhakikisha zinawachukua wanafunzi huku yeye akiahidi kuchukua wanafunzi watano kila mwaka kwenye ofisi yake.

“Kila mwaka ofisi yangu itatoa nafasi ya field (mazoezi kwa vitendo) kwa wanafunzi watano na ninakuomba mkuu wa chuo uniletee wanafunzi wenye maadili,wazalendo na wenye weledi”alisisistiza.

Aidha Dk Abbas ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –Maelezo aliwataka wahitimu kufanya kazi kwa uzalendo na kukosoa baadhi ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali. “Dhima kubwa ya wanahabari ni kuwa mlinzi wa kiona mbali cha jamii,” alisema.

Katika mahafali hayo, Dk Abbas aligusia utekelezaji wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ikiwamo ya reli ya kisasa Standard gage (SGR) pamoja na kulifufua shirika la ndege la Tanzania kwa kununua ndege ya Airbus A220 ambayo niya kwanza Afrika.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Joachim Rupepo alisema kuwa chuo kimetoa wataalamu wenye uwezo wa kujiajiri na wenyembinu mbadala na kueleza kuwa malengo ya chuo ni kuisaidia Serikali kutoa mafunzo ya ufundi.

“Chuo kimetoa wataalamu wenye uwezo wa kujiajiri na wenye mbinu mbadala, moja ya malengo ya chuo chetu ni kuisaidia serikali kutoa elimu ya mafunzo ya ufundi,”alisema.

Aidha aliwaasa wahitimu kufanyakazi kwa weledi ili kuijengea taasisi yao heshima, kwa kutumia ujuzi walioupata chuoni kujiajiri bila kubweteka kusubiri ajira ya serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles