26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanne kortini kwa utakatishaji fedha


PATRICIA KIMELEMETA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapandisha kizimbani watu wanne na kusomewa mashtaka manne yakiwamo ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 83.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Dar es Salaam ni Omary Guya (27), Godlisten Sammast (33), Froliana Kagisa (27) na Justine Bukuku (28).

Wakili wa Serikali, Grolia Mwenda, aliwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Maila Kasonde na kudai kuwa kati ya Machi na Aprili 6, mwaka huu jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Alidai kuwa katika tarehe hizo eneo la yadi iitwayo Uganda iliyopo Bandari ya Dar es Salaam, waliiba gari aina ya Toyota VXR-V8 yenye thamani ya Sh 404,769,692 mali ya Kampuni ya  Toyota Tanzania.

Alidai washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Aprili 11 na 12, mwaka huu wakiwa na nia ya kudanganya walijipatia Sh milioni 83 kutoka kwa Godfrey Kundi, wakidai kwamba wamiliki wa gari hilo huku wakijua si kweli.

Wanadaiwa kuwa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, walitakatisha gari hilo kwa kuliuza Sh miolini 83 huku wakijua gari hilo limetokana na kosa la wizi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Mwenda, alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Kasonde, aliwaeleza washtakiwa hao kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu uchumi na hawaruhusiwi kujibu chochote hadi mahakama hiyo itakapopata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Alidai moja ya shtaka linalowakabili ni la utakatishaji fedha ambalo halina dhamana, hivyo washtakiwa wote watabaki rumande hadi Mei 17, mwaka huu itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles