25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi ya Shamim, mumewe haujakamilika

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

UPELELEZI wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45), haujakamilika.

Upande wa Jamhuri ulidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilikuwa inatajwa.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, alidai mbele ya  Hakimu Mkazi wa Mfawidhi, Kelvin Mhina, kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine.

Baada ya kudai hayo, Wakili wa Utetezi, Charles Kisoka na Hajra Mungula, walidai kuwa shauri hilo halina dhamana, hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Wakili Wankyo alidai kuwa, amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019 na washtakiwa walirudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.

Shamim na mumewe, wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei mosi, mwaka huu wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles