24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo awatoa wasiwasi Juventus

LISBON, URENO

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuumia mapema wiki hii akiitumikia timu ya taifa Ureno kwenye michuano ya kuwania kufuzu Euro 2020.

Katika mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, lakini mchezaji huyo hakumaliza dakika 90 kutokana na kuumia nyama za paja na kuwaweka wasiwasi mashabiki wa Juventus kuelekea michezo yao mbalimbali ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba, japokuwa alitolewa kwenye mchezo huo, lakini hana tatizo kubwa la kutisha na kumfanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

“Sina wasiwasi kwa kuwa ninaujua vizuri mwili wangu, haya yanatokea kwenye soka, hivyo ninaamini ninaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki moja au mbili, nitakuwa imara.

“Najua mashabiki wana hofu, lakini nataka kuwatoa wasiwasi kwamba nitarudi viwanjani siku za hivi karibuni,” alisema mshambuliaji huyo.

Ronaldo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Juventus tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita.

Mchango wake umeifanya Juventus kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwaondoa Atletico Madrid. Mchezo wa kwanza Atletico Madrid walifanikiwa kushinda mabao 2-0, huku mchezo wa mwisho wa marudiano Ronaldo aliifungia Juventus mabao matatu katika ushindi wa 3-0 na kuifanya timu hiyo kufuzu, ambapo inatarajia kukutana na Ajax, Aprili 10, mwaka huu.

Endapo hali ya mchezaji huyo itakuwa bado haiko sawa ndani ya wiki mbili, basi ataukosa mchezo huo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Ajax. Timu hiyo ya Ajax imefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuwaondoa wababe wa michuano hiyo Real Madrid, hivyo timu hiyo inaonekana kuwa tishio kubwa msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles