29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mawaziri wa JPM watoa somo kwa watumishi

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WATUMISHI wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, Sera, Bunge na Uwekezaji,  wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kwa  makini katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na ufanisi wa hali ya juu.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama pamoja na mwenzake wa ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki, walipofungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha ofisi hiyo   jijini Dodoma.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa ufanisi kwa sababu  hakuna haki pasipo wajibu.

“Hivyo kila mtumishi azingatie hayo ili kuwa na utendaji wenye manufaa kwa ofisi na Serikali kwa ujumla,” alisema Mhagama.

Waziri Mhagama ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za  nidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi ikiwamo watumishi wazembe na wenye tabia ya kuchelewa kazini.

Naye Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji, Angellah Kairuki aliwapongeza watumishi wa ofisi hiyo kwa mafanikio yanayoonekana.

Alitoa wito kwa watumishi kuendeleza jitihada hizo ili kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.

“Kipekee niwapongeze watumishi kwa kuendelea kutekeleza vizuri majukumu ya kila siku kwa weledi kwa kuzingatia ukubwa wa ofisi hii.

“Tuendelee kutekeleza vya ufanisi kuvutia wawekezaji nchini waweze kuona fursa na kuwekeza,” alisema Kairuki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles