26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yakerwa kulindwa gaidi


WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imeamua kuikosoa vikali ile ya Ujerumani kwa uamuzi wa kumrejesha nchini Uturuki, Adem Yilmaz ambaye alihukumiwa kifungo cha gerezani kwa makosa ya kujihusisha na ugaidi. Ujerumani ilichukua hatua hiyo licha ya ombi la Marekani kutaka apelekwe nchini humo.

Yilmaz alirudishwa nchini kwake Uturuki mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutumikia kifungo cha miaka 11 Ujerumani kwa kosa la kupanga shambulizi la bomu mwaka 2007 dhidi ya raia wa Marekani wanaoishi nchini Ujerumani.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Matthew Whitaker, amesema nchi yake imesikitishwa na hatua ya Ujerumani kumrejesha Yilmaz nchini Uturuki.

Amesema Ujerumani imemsaidia kwa makusudi Yilmaz kukimbia mkono wa sheria kwa kumweka kwenye ndege na kumpeleka Uturuki.

Marekani iliomba Yilmaz apelekwe nchini humo ili akajibu mashtaka ya ugaidi baada ya kuandaa kwa siri shambulizi karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan mwaka 2008, lililowaua wanajeshi wawili wa Marekani na kuwajeruhi watu wengine 11.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles