30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Disko toto, vigodoro marufuku Dar

GRACE SHITUNDU – DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limejipanga kukabiliana na vitendo vyote vinavyoashiria uhalifu.

Pia limepiga marufuku shughuli za disko toto na ngoma za vigodoro huku likitoa onyo kwa waendesha bodaboda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema wamejipanga kuimarisha doria katika kipindi chote cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Alisema kwa kushirikiana na kampuni binafsi, Jeshi la Polisi litaimarisha ulinzi katika sehemu zote zitakapofanyika ibada na mikesha ya Krismasi na Mwaka Mpya.

“Katika kuimarisha doria tutakuwa na askari watakaotembea kwa mguu, farasi, mbwa, pikipiki, magari pamoja na helkopta kuhakikisha maeneo yote ya Dar es Salaam yanaendelea kuwa salama.

“Mwaka jana tulisherehekea vizuri Krismasi na Mwaka Mpya na hakukuwa na uhalifu kabisa, tulivyoanza mwaka 2018 hadi leo (jana) Desemba 22 hali iko shwari na tumeimarisha ulinzi, na ushirikiano huu uendelee ili tuweze kumaliza mwaka kwa mafanikio,” alisema.

Mambosasa alisema wakati wa sikukuu wanaendelea kuwatahadharisha wazazi kuwa makini na kusherehekea na watoto wao pamoja ili kuepusha matukio yaliyotokea kipindi cha nyuma.

Kuhusu disko toto, alisema hawatarajii kuwepo kwa kuwa hadi sasa hakuna watu walioomba kibali.

“Hadi sasa hatujapata mtu aliyeomba kibali cha kuendesha disko toto ili vyombo vya usalama waweze kufanya ukaguzi mapema kuona kama eneo litakaloombewa linafaa kwa shughuli hiyo kwa watoto wadogo,” alisema.

Aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto  kutoviendesha wakati wamelewa ili kuepusha ajali wakati wa sikukuu hizo.

Kuhusu ngoma za vigodoro, alisema hazina maadili na katika maeneo mbalimbali huzicheza wakiwa wamevaa nguo zinazoonesha maumbile.

“Katika maeneo yetu kuna watoto wanapoziona wanajifunza mambo yanayofanywam hivyo jeshi litawashughulikia kabla hawajaanza kucheza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles