31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ujumbe wa Gigy Money wazua gumzo

Mwandishi Wetu

MREMBO anayefanya vyema kwenye filamu na muziki nchini, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amewashtua mashabiki zake baada ya kudai anatamani kufa bila sababu.

Gigy Money, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huo ambao  aliufuta baada ya muda mfupi akidai kukumbwa na hali ya kutotamani kula, kulala na anajichukia.

 “Natamani kufa bila sababu yoyote, siwezi kula wala siwezi kulala kwa kifupi najichukia mwenyewe na nimekuwa dhaifu, yaani inauma ila inabidi uwe mkubwa kuelewa, sipo ‘interested’ na mtu yeyote yule wote wamenishinda,” alisema Gigy Money ambaye hivi karibuni aligombana na kumtimua nyumbani kwake na mpenzi wake raia wa Nigeria, Hunchy Huncho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles