|Nairobi, Kenya
Naibu Jaji Mkuu nchini Kenya, Philomena Mwilu, amekamatwa katika mahakama ya juu jijini Nairobi kutokana na tuhuma za rushwa na ufisadi.
Jaji Mwilu, amechukuliwa katika Mahakama Kuu na Kurugenzi ya Mashtaka ya Jinai na wapelelezi kutoka kwenye Uongozi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) kwa madai ya kuhusishwa na kufilisika kwa Benki ya Imperial.
Mwilu amepelekwa katika Makao Makuu ya Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu, kwa mahojiano.
Muda mfupi baada ya kukamatwa, mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Noordin Haji, ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo.