24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 13, 2024

Contact us: [email protected]

Maajabu ya karafuu katika mwili wa mwanadamua

karafuu

Na Mwandishi Wetu,

KARAFUU ni zao linalotokana na mkarafuu. Zao hili halimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu kwa maisha ya binadamu.

Zao hili lina matumizi mengi, ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula na vinywaji, dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.

Pia hutumika katika uzalishaji wa bidhaa nyingine ikiwamo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengeneza dawa za meno na manukato.

Karafuu hutumika kwenye vyakula mbalimbali ikiwamo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu kama vile vileja, beskuti na donat na kwa upande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa.

wataalamu wanasema kuwa karafuu husaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo, ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani yake.

Aidha, hutumika katika utengenezaji wa mafuta ambayo husaidia kusafisha damu. Tafiti zinaonyesha kuwa vinasaba vilivyomo katika karafuu vinapunguza sumu katika damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu.

Pia karafuu hutumika katika viwanda kwa ajili ya kutengezea dawa za meno kwa ajili ya kutunza meno na kuondosha maumivu ya meno na fidhi, kung’arisha meno na kuleta harufu nzuri ya kinywa, harufu iliyomo katika karafuu husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni.

Karafuu pia inatajwa kusadia kutibu vidonda vya mdomo na kuimarisha afya ya fizi pamoja na kuzuia meno kuoza.

Madaktari wa meno wamekuwa wakitumia mafuta ya karafuu kwa ajili ya kutibu matatizo ya meno, hii ni kwa sababu mafuta hayo yamekusanya vinasaba vya eugnol ambavyo ni vizuri kwa meno na fidhi.

Karafuu inatumika katika urembo… wanawake hupenda kusugulia mwili (scrub) kwa kuchanganya unga wa karafuu kavu iliyosagwa na mafuta ya nazi na liwa ambapo husuguliwa mwili mzima kwa ajili ya kuondoa uchafu na kuufanya mwili kuwa nyororo.

Sabuni zinazotengenezwa kwa karafuu huondoa harara, vipele na chunusi na hivyo kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kuvutia.

Matumizi ya karafuu na mafuta yake humfanya mtu kuwa mchangamfu… humwondolea uchovu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri nakufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.

Mafuta ya karafuu yanapochanganywa na chumvi, husaidia kuondosha maumivu ya kichwa, matatizo katika mfumo wa upumuaji, kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles