23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madini mapya yagundulika huko Mererani,Manyara

1-closeupofthe

Madini mapya yamegunduliwa katika eneo la Mererani katika milima ya Lelatema wilayani Simanjiro, Manyara na kupewa jina Merelaniite.

Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yamepatikana, ambalo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite.

Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia cha London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian ya Washington, Marekani.

Kwa mujibu wa wataalamu waliogundua madini hayo, wanasema yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12.

Madini hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite, chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite, graphite, alabandite na wurtzite.

Kwa mujibu wa John Jaszczak, mwanafizikia aliyeongoza katika utafiti huo, madini hayo mapya yametambuliwa na taasisi inayoyapa majina madini, IMA CNMNC (2016-042), na kupewa jina linalotokana na eneo yalipogunduliwa kwa heshima ya wachimba migodi wa eneo hilo wa zamani, wanaoishi na wanaofanya kazi.

Madini hayo yalitambuliwa mara ya kwanza mwaka 2012 na Simon Harrison na Michael Wise, bila wataalamu hao kuyafahamu vyema, pale walipogundua vitu vilivyoonekana kama nyaya ndogo zilizokuwa zimedunga na kuingia ndani ya vipande vya madini ya chabazite. Source: BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles