30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Zungu: CCM itaamua Spika wa Bunge

azani+zunguNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE mteule wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM) amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia mbio za kuwania Spika wa Bunge hadi chama chake kitakapotoa utaratibu.

Amesema pamoja na baadhi ya makada wenzake wa CCM kuanza kujipitisha   kuwania nafasi hiyo  kwake anaamini  CCM ndicho kitatoa utaratibu wa kupatikana spika.

Zungu alitoa kauli hiyol Dar es Salaam jana alipozungumza na MTANZANIA baada ya jina la mwanasiasa huyo kutajwa katika  kuwania uspika wa Bunge.

Alisema yeye hajawahi kutamka kuwania nafasi hiyo zaidi ya wabaya wake wa siasa kutumia jina lake kwa malengo wanayojua wao.

“Mimi bado sijatamka kwa kinywa changu kama ninataka kuwania uspika ila utaratibu wa jambo hili utatolewa na chama.

“Hivyo  kama unataka kujua nitawania ama laa subiri kwanza chama kitoe utaratibu ndipo nitakuwa na la kusema lakini kwa sasa hapana.

“CCM ni chama tawala kina utaratibu wake nitakuwa mtu wa ajabu kusema nitawania kuwa Spika wa Bunge wakati hata chama hakijatoa utaratibu,” alisema Zungu.

Hata hivyo, alisema  anajivunia namna bora anavyotekeleza ilani ya CCM kwa wapiga kura wake wa Ilala.

Alisema  kila mara wamekuwa msaada mkubwa kwake na wameendelea kumuamini kwa kumchagua tena.

Zungu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge katika Bunge la 10 ni miongoni mwa  wenyeviti wanaosifika kwa rekodi ya kuendesha vizuri Bunge.

Anatajwa kama kiongozi anayepewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na chama chake cha CCM kuwania nafasi hiyo ya Spika wa Bunge ikiwa ataridhia kufanya hivyo.

Baadhi ya wabunge wa CCM na hata vyama vya upinzani wamekuwa wakimtaja mbunge huyo wa Ilala kama ni moja ya nguzo ya Bunge na hana upendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles