31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Zungu achangiwa fomu ya ubunge Ilala

ZunguNa Jonas Mushi, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la wanafunzi wa Elimu ya Juu la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, limesema linaridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ilani wa Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM).
Kutokana na hali hiyo wanafunzi hao waliendesha harambee na kukusanya Sh 75,000 ambazo walimkabidhi mbunge huyo kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumza juzi katika semina ya itikadi ya kujadili utekelezaji wa ilani ya CCM, Mwenyekiti wa Seneti Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam, Imani Matabula alisema pamoja na hati hiyo, chama hicho kimejipanga vema kuhakikisha Ilala na majimbo mengine yanarudi katika himaya ya CCM.
Alisema hatua ya Zungu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge, ni ya mapinduzi na anastahili kuungwa mkono na kila mwana CCM.
Awali Mbunge huyo wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, alisema lazima vijana hao wa CCM watambue lengo kuu la chama ni kukamata na kushikilia madaraka yoyote.
Alisema kutokana na hali hiyo vijana wasikubali kutumiwa ili kuiondoa CCM madarakani kwa kudanganywa kwa sababu mambo yatabadilika ikizingatiwa hakuna serikali ambayo haina changamoto.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alimpongeza Mbunge Zungu kwa kuwa ni mmoja wa wabunge wanaojitoa kusaidia maendeleo katika majimbo yao.
Kinana aliyasema hayo alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri ya Chamwino mjini hapa.
“Kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakitumia fedha zao kusaidia kusukuma kasi ya maendeleo katika majimbo yao bila kujali kusubiri fedha za Serikali akiwamo Zungu.
“CCM inawapongeza wabunge wa aina hii wanaotumia rasilimali zao ikiwamo mishahara yao kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wao,” alisema Kinana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles