26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZUMA AZUIWA KUHUDHURIA MAZISHI

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI


RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma hatahudhuria mazishi ya mwanaharakati wa kuipinga serikali ya ubaguzi wa rangi Ahmed Kathrada kwa ombi la familia yake.

Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu mwaka uliopita, kufuatia kashfa za ufisadi.

Aidha mke wa Kathrada, Barbara Hogan anafahamika kuwa mkosoaji mkubwa wa Zuma. Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa ataiwakilisha serikali kwenye mazishi hayo.

Kathrada (87) aliyefariki dunia juzi, alifungwa pamoja na shujaa wa Afrika Kusini Nelson Mandela kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.

Alitumikia kifungo cha miaka 26 gerezani kabla ya kaachiwa huru mwaka 1989. Baadaye alihudumu kama mshauri Rais Mandela, kwenye serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia.

Zuma alikuwa ameagiza bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo chake, na kuahirisha mkutano wa mawaziri ili maafisa wapate kuhudhuria mazishi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles