29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Zouma kuikosa Ligi Kuu England

Kurt-Zouma-Net-WorthLONDON, ENGLAND

BEKI wa klabu ya Chelsea, Kurt Zouma, atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki iliyopita.

Zouma atafanyiwa upasuaji kwenye goti lake ambalo aliumia kwenye Uwanja wa Stamford Bridge baada ya kutua vibaya aliporuka juu kupiga mpira kwa kichwa.

Uchunguzi umethibitisha kwamba, aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji ili kuweza kutibu tatizo hilo.

Kutokana na hali hiyo, beki huyo atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima na kukosa michezo yote ya Ligi Kuu ambayo imebakia pamoja na michuano ya Euro ambayo inatarajia kufanyika Juni 10 hadi Julai 10 mwaka huu nchini Ufaransa.

Kupitia akaunti ya Twitter ya mchezaji huyo amewashukuru mashabiki wote ambao wamemtumia ujumbe wa kumpa pole na kumuombea aweze kurudi uwanjani mapema iwezekanavyo.

“Ninaushukuru uongozi wa klabu yangu kwa ushirikiano waliouonesha pamoja na mashabiki wangu wote, ninaamini nitakuwa vizuri haraka iwezekanavyo kwa kuwa ninatarajia kufanyiwa upasuaji saa 48 kuanzia sasa,” aliandika Zouma.

Hata hivyo, klabu hiyo imemtakia kila la heri mchezaji huyo aweze kupona mapema huku wakitegemea kuungana naye msimu ujao.

Kutokana na kuumia kwa Zouma, sasa Chelsea katika safu ya ulinzi itakuwa inaundwa na John Terry huku nafasi ya Zouma ikichukuliwa na Gary Cahill katika kipindi hiki chote cha msimu huu.

Zouma ambaye amekuwa kama pacha wa John Terry katika safu ya ulinzi uwanjani, ameichezea Chelsea mechi 32 msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles