24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMBABWE YAALIKA NCHI 46 KUANGALIA UCHAGUZI MKUU

HARARE, ZIMBABWE


SERIKALI ya Zimbabwe imepitisha orodha ya nchi 46, jumuiya za kikanda na za mabara 15 kuangalia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Julai.

Hatua hiyo inaashiria dhamira ya utawala wa Rais Emmerson Mnangagwa kutimiza ahadi ya kuendesha chaguzi huru, wazi na haki na kuachana na utaratibu wa nyuma wa kuzuia baadhi ya mataifa, hasa ya Magharibi.

Seneta wa Arizona, Jeffrey Lane Flake, ambaye yupo katika Kamati ya Uhusiano wa Kigeni nchini Marekani na Mbunge wa zamani nchini humo, Andrew Jackson Young Junior, ni sehemu ya watu mashuhuri walioalikwa.

Nchi zilizoalikwa ni pamoja na wanachama wote 15 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC) na wanachama wote wa Umoja wa Ulaya (EU).

Katika bara la Amerika Kaskazini, zilizoalikwa ni Marekani, Canada na Mexico huku Brazil, Ecuador, Nicaragua na Venezuela zikialikwa kuiwakilisha Amerika ya Kusini.

Asia zilizoalikwa ni China, India, Indonesia, Iran, Japan, Malaysia, Pakistan, Palestina, South Korea na Thailand huku Cuba, Jamaica, Trinidad and Tobago, Guyana na Barbados zikiwakilisha Visiwa vya Caribbean.

Australia, New Zealand na Papua New Guinea pia zimealikwa.

Aidha vyama vya ukombozi kama vile ANC (Afrika Kusini), CCM (Tanzania), FRELIMO (Msumbiji), BDP (Botswana) na MPLA (Angola) pia ni miongoni mwa waangalizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles