25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ZIDANE: RONALDO, RAMOS WAMEMALIZA TOFAUTI ZAO

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Zinedine Zidane, ameweka wazi kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo na nahodha Sergio Ramos, wamemaliza tofauti zao.

Uongozi wa klabu hiyo uliwakutanisha wachezaji hao juzi, kabla ya kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi Kuu nchini Hispania.

Sababu za wawili hao kuwa kwenye mgogoro ni baada ya Real Madrid kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Novemba 1, kwenye Uwanja wa Wembley, hivyo Ronaldo akatupia lawama kwa uongozi wa klabu hiyo kwa kudai kwamba, walifanya makosa makubwa kuwauza wachezaji wao, James Rodriguez na Alvaro Morata.

Kauli hiyo ya Ronaldo ilionekana kumchukiza sana Ramos na ndipo nahodha huyo alisema kuwa, Ronaldo ni mchezaji mbinafsi sana na hakupaswa kuongea kauli kama hiyo na alitakiwa kushirikiana na wenzake ili kuisaidia timu.

Hata hivyo, baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa, Ronaldo aliweka wazi kuwa, hana mpango tena wa kuendelea kuwa na timu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake.

“Ni wazi kwamba Sergio Ramos ni miongoni mwa wachezaji wenye akili sana ndani na nje ya uwanja, anaweza kumwambia kitu mchezaji yeyote hata kama ni Cristiano Ronaldo, isitoshe wachezaji hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na wamezoeana.

“Mchezaji huyo alistahili kumwambia hivyo Ronaldo kutokana na kauli yake, lakini ukweli ni kwamba kila kitu kipo sawa kwa sasa, uongozi wa klabu uliamua kukaa pamoja na wachezaji hao kwa ajili ya kumaliza tofauti zao na kila kitu kinakwenda sawa sasa.

“Kwa pamoja naweza kusema nina wachezaji wawili kwenye kikosi ambao wanatengeneza historia ndani ya timu hii, wamekubali kumaliza tofauti zao ili kuweza kuipigania timu yao katika michezo inayofuata,” alisema Zidane.

Wababe hao wa soka barani Ulaya, msimu huu wanaonekana kuwa wameuanza vibaya kutokana na kiwango chao na ushindi wanaoupata, huku baadhi ya mshabiki wakidai kuwa, mshambuliaji wao huyo ambaye ana tuzo nne za Ballon d’Or, amekuwa kwenye kiwango cha chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles