32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

ZIDANE: MKATABA WANGU HAUNA MAANA MADRID

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane, amefunguka na kusema mkataba wake ndani ya klabu hiyo hauna maana yoyote endapo timu yake inashindwa kufanya vizuri katika baadhi ya michezo yake.

Klabu hiyo juzi ilishuka dimbani kwenye michuano ya Kombe la Copa del Rey dhidi ya Numancia na kutoka sare ya 2-2, lakini Madrid tayari imefanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa mabao 3-0, hivyo kuwa jumla ya mabao 5-2.

Katika mchezo wa juzi, Madrid walitoa sare hiyo huku nyota wao, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakiwa nje ya uwanja na mabao ya Madrid yakiwekwa wavuni na Lucas Vazquez.

Lakini kocha huyo amedai kwamba, japokuwa alisaini mkataba mpya  Septemba mwaka jana, bado hauna maana kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri.

“Nimekuwa nikipambana katika kila mchezo, lakini ushindani umekuwa mkubwa sana, sina uhakika kama nitaendelea kuwa hapa kwa miaka mitatu au minne kutokana na mwenendo wa timu hii.

“Bila ya kujali mkataba wangu, lakini lazima nifanye kile ambacho viongozi wa timu hii wanakitaka, kinyume na hapo lazima mambo yatakuwa tofauti.

“Bado nina furaha na wachezaji nilionao na kile ambacho wanakifanya, kikubwa ni kuongeza juhudi na kupambana kwa kuwa ushindani ni mkubwa sana,” alisema Zidane.

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo Januari 2016 na kuweka historia mpya ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo pamoja na kutwaa Ligi Kuu nchini Hispania, lakini kwa sasa amekuwa kwenye ushindani mkubwa na kuifanya timu hiyo iwe kwenye wakati mgumu.

Kwenye msimamo wa Ligi nchini Hispania, Real Madrid inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 32, wakati huo wapinzani wao Barcelona wakishika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 48 baada ya kucheza michezo 18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles