29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

ZIC yadhamiria kuwaunga mkono Wanawake Wajasiriamali Mtwara

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

SHIRIKA la Bima la Zanzibar (ZIC) limedhamiria kujitolea kudhamini Tamasha la Wajasiriamali Wanawake mkoani Mtwara linalotarajiwa kufanyika Septemba 19, mwaka huu mkoani humo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Arafat Haji, amesema baada ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya na kufanya mazungumzo, ZIC imekuwa ikitoa huduma katika Mkoa huo hivyo ni wakati wa kurejesha kwa wateja wao.

“Tulikua tunatoa huduma zetu hapa Mtwara hivyo tuna njia nyingi za kurejesha kwa jamii hususan wateja wetu na hata wasio wateja wetu na tumehaidi kuwepo katika Tamasha la wajasiriamali wanawake ambapo kimsimgi kuwaunga mkono wanawake,” amesema.

Hata hivyo, Haji ameeleza kuwa katika Tamasha hilo wataweza kutoa elimu kwa wanawake hao wajasiriamali kwa namna gani wataweza kujilinda na kutumia bima kwa maslahi ya familia zao pamoja na biashara zao kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles