28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Zara Tours yaweka rekodi nyingine yakupandisha wageni wengi zaidi Mlima Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Kampuni ya Utalii ya Zara Tours ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mara nyingine tena imeingia katika historia mpya kupandisha wageni wengi katika mlima Kilimanjaro, ambapo zaidi ya wapanda mlima 228 wakiwemo mabalozi zaidi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wameshiriki kampeni hiyo ya Twenzetu kileleni ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizugumza leo Desemba 7, mara baada hafla ya kuwaaga wapanda mlima 228 katika geti la Marangu Mkurugenzi wa kampuni ya Zara tours Adventures, Zainab Ansell amesema tangu kuanza kwa kampeni hiyo ya Twende Zetu kileleni kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika kuwekua mwamko mkubwa.

Amesema ni takriban zaidi ya miaka 15 iliyopita wakati wa Generali Waitara.

Amesema ni jambo la kujivunia kusema kuwa tumefanikiwa kufanya mpaka leo kwani Twende Zetu Kileleni ya mwaka huu imefanikiwa kutokana na idadi kubwa ya watu kushiriki zoezi hilo.

Amesema kampeni ya mwaka huu imekuwa ya aina yake huku akieleza furaha yake kutokana na watu mashuhuri wakiwemo mabalozi zaidi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kushiriki.

“Kwa kweli ni furaha kubwa sana kuona mwamko mkubwa kiasi hiki hadi mabalozi wetu wamekuja kupanda mlima ikiwa ni maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika,naamini kampeni hii itaendelea kuleta mwamko mkubwa wa watalii kuendelea kuja kupanda mlima Kilimanjaro,”amesema.

Amesema mwamko huo umetokana na juhudi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hasan kupitia kampeni yake ya Royal Tours imeleta mabadiliko makubwa nasisi kama wadau wa utalii tutaendele kuunga mkono juhudi za Serikali, kwa kutoa huduma bora kwa wageni wanakuja kwa ajili kutembea vivutio mbalimbali.

“Mafanikio ni makubwa sana na faida kubwa ipo kwani filamu ya mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeleta matunda makubwa sana kwani watanzania wengi wameonesha mwamko kufanya utalii wa ndani na wameendelea kujitokeza na kupanda mlima Kilimanjaro,” amesema.

Amesema anajivunia kuwa na timu makini na vijana wanaojituma katika kufanya kazi wakiwemo wagumu ambao hufanya kazi kwa weledi.

Mkuu wa wilaya Moshi, Kisare Makore amesema kuwa tangu mwaka 1961 mpaka leo ni miaka 11 na pia amewapongeza wamabalozi kujitoa kutangaza vivutio vya utalii nchini ambapo aliwasisitiza kuendelea kutangaza utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro.

Amesema: “Kupanda mlima, siyo adhabu bali ni jambo la furaha, hivyo pandeni kwa lengo la kuutangaza mlima Kilimanjaro na kupanda Kwa kufuata ushauri wataalam hususan waongozaji ili zoezi hili liweze kufanikiwa,”.

Katika hatua nyingine Makore ametoa wito kwa wananchi wanaoishi katika Mwambao wa Pwani kuona wana wajibu wa kuhifadhi maeneo yao ili kuhifadhi na kuendeleza uwepo wa theluji katika Mlima Kilimanjaro.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi nchini, Herman Batiho amesema wapanda Mlima hao wamepanda kupitia mageti matatu yakiwemo Geti la Lemosho, Machame na Marangu na wote watakutana katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Desemba 9,2023 huku wakipandasha Bendera ya Tanzania siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi 11 wanaowakilisha Nchi ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali, Amidi wa muda wa Mabalozi hao, Maadhi Maalimu amesema wajibu wao mkubwa walionao ni kulinda na kutetea maslahi ya nchi na, kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini (TANAPA) Jenerali Mstaafu George Waitara amesema wameboresha huduma ndani ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwemo Mawasiliano, vyoo, Nyumba pamoja na miundombinu ya barabara.

Jumla ya watu 228 wamepanda Mlima Kilimanjaro yakiwemo makundi mbalimbali kama vile Taasisi za Umma, Taasisi binafsi, Wasanii, Mabalozi pamoja Wanahabari huku lengo kuu ni kupandisha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima Kilimanjaro katika kuelekea miaka 62 ya Uhuru ifikapo Desemba 9,2023.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles