28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Zanzibar mbioni kufikia vigezo vya WHO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekitki wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekitki wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitki wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema, katika miaka michache ijayo, Zanzibar itakuwa na madaktari wa kutosha kufikia uwiano uliopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) wa angalau daktari mmoja kuhudumia wagonjwa 10,000 kwa nchi zinazoendelea.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya  Udaktari ya Zanzibar inayoendeshwa kwa ushirikiano na Chuo kikuu cha Matanzas cha Cuba yaliyofanyika katika Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni mjini Unguja.

Katika mahafali hayo wanafunzi wa udaktari 38 ambao walichukua mafunzo yao hapa Zanzibar na nchini Cuba walikabidhiwa shahada zao za udaktari kutoka kwa Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Matanzas Dk. Luis Ulpiano Perez Marques.

Dk. Shein alisema kuhitimu madakatari hao 38 kwa mpigo ni ushahidi wa kutosha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikitekeleza kwa vitendo azma yake ya kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya.

Alifafanua kuwa mwanzoni mwa mwaka huu uwiano wa daktari kwa idadi ya watu ulikuwa ni daktari mmoja kwa wananchi 18,982 lakini kuhitimu kwa madaktari hao kumeleta mabadiliko katika uwiano huo.

Hata hivyo alisema katika kipindi kifupi kijacho vijana wengi waliopelekwa kusomea udaktari nchi za nje pamoja na Tanzania Bara watamaliza masomo yao hivyo kuongeza idadi ya madaktari na hivyo kupunguza pengo la uwiano huo.

Awali akitoa maelezo katika mahafali hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Saleh Mohamed Jidawi, alisema mafunzo hayo yamegharimiwa kwa kiwango kikubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles