29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

ZAMBIA WAHAMASISHWA KUTUMIA BANDARI DAR

Na MWANDISHI WETU-ALIYEKUWA LUSAKA

WAFANYABIASHARA na wadau wengine nchini Zambia wamehimizwa kuendelea kutumia bandari za Tanzania hasa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuboreshwa kwa huduma zake.

Akizungumza na wadau wa kampuni za madini na wafanyabiashara kutoka miji ya Kitwe, Ndola na jijini Lusaka nchini Zambia, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, alisema Serikali imeshaondoa vikwazo katika Bandari ya Dar es Salaam na reli ya Tazara ili kuongeza ufanisi.

Alisema kijiografia, Bandari ya Dar es Salaam bado ni kivutio kikubwa kwa nchi jirani mbali na mabadiliko makubwa ya kimuundo na uongozi yaliyofanywa hivi karibuni ili kuifanya ya kisasa zaidi.

Akitoa mifano ya maboresho yanayoendelea kufanywa, alisema mradi wa upanuzi wa magati 1-7 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadau wengine unatarajiwa kuanza rasmi Aprili mwaka huu.

“Baada ya kumalizika kwa mradi huu mapema mwaka huu, bandari itakuwa na uwezo mkubwa wa kuhudumia meli kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa, lakini pia TPA inaendelea kuweka vifaa vya kisasa vitakavyoiwezesha kwenda na teknolojia ya kisasa.

“Aidha, reli ya Tazara uwezo wake umeongezwa kwa kununua mabehewa zaidi na hivyo kuongeza idadi ya safari kati ya Bandari ya Dar es Salaam na miji ya Lusaka, Kitwe na Ndola hadi kufikia safari sita kwa wiki,” alisema.

Wakati wa ziara hiyo, ujumbe wa TPA ulikutana na wadau muhimu na wafanyabiashara katika miji hiyo na kusikiliza maoni na changamoto wanazopata ambapo Injinia Kakonko alitumia fursa hiyo kuwashukuru kutokana na kuridhishwa na ushirikiano wao na kuahidi kuzifanyia kazi haraka changamoto zenu ili kuboresha huduma na mazingira ya biashara kati ya nchi hizo.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma, aliwasisitiza wafanyabiashara wa nchi hiyo kutumia huduma za ubalozi huo ili kukwepa matapeli na watu wasio waaminifu.

“Ni kupitia ubalozi wetu ndipo mtapata orodha ya kampuni halali mnazoweza Na MWANDISHI WETU

-ALIYEKUWA LUSAKA

“Ni kupitia ubalozi wetu ndipo mtapata orodha ya kampuni halali mnazoweza kuzitumia kwa kazi zenu,” alisema balozi huyo.

 kwa kazi zenu,” alisema balozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles