Tunis, Tunisia
Shirika la kimataifa la msaada wa kiutu la Msabala Mwekundu imetoa ripoti ya vifo 23 vya waafrika wahamiaji kilichotokea kwenye bahari ya Mediterrania baada ya kuzama kwa boti ilikuwa ikitokea Libya kuelekea Italia.
Shirika hilo limesema boti hiyo iliyozama ilikuwa na zaidi ya wahamiaji 90 na jeshi la nchi ya Tunisia limefanikiwa kuwaokoa wahamiaji 70 pekee huku 23 wakipoteza maisha.
Pia katika tukio jingine, shirika la Msalaba mwekundu limesema jeshi la Tunisia limewaokoa wahamiaji 39 waliokuwamo kwenye boti nyingine ya mpira iliyozama nje kidogo ya pwani ya Tunisia.
Katika wiki za karibuni zaidi ya wahamiaji 120 wamezama na kupoteza maisha kwenye pwani ya Tunisia kufuatia kuongezeka kwa safari za kutoka Tunisia na Libya kuelekea barani Ulaya kwa madai ya kutafuta maisha mazuri.