25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera kuamua hatma ya Yanga Kagame

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM 

UONGOZI wa Yanga umesema hatma ya ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), wameiacha kwa kocha wao Mwinyi Zahera.

Yanga ni miongoni mwa timu tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara  zilizopata mwaliko wa kushiriki michuano hiyo, iliyopangwa  kuanza Julai 4 nchini Rwanda.

Nyingine ni Simba ambaye ni bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Azam FC.


Hata hivyo, Simba imeweka wazi msimamo wake kwamba haitashiriki michuano hiyo, ikikusudia kuweka  nguzu zake katika maandalizi ya Ligi Kuu msimu ujao na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Michuano hiyo ya inayoandaliwa na Baraza la Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Paul Kagame, inatarajia kuanza kutimua vumbia Julai 4, jijini Kigali, Rwanda.

Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka 2015 na Azam FC kutwaa ubingwa huo, baada ya kuitungua Gor Mahia mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bingwa wa michuano hiyo uvunakitita cha Dola za Kimarekani  30,000 (zaidi ya Sh milioni 68 za Kitanzania) kutoka kwa mdhamini mkuu wa michuano hiyo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame .

Yanga ambayo ni mabingwa mara tano wa michuano hiyo, imeamua kumkabidhi jukumu la kumua ushiriki wa timu hiyo Zahera, ambaye kwa sasa yuko katika maandalizi fainaliza Mataifa Afrika (Afcon)  zitakazofanyika wiki mbili zijazo nchini Misri.

Zahera mbali ya kuinoa Yanga, pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC), akimsadia kocha Frolent Ibenge, ambaye anainoa AS Vita inayoshiriki Ligi Kuu ya taifa hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alithibitisha klabu yake  kupokea mwaliko huo, lakini akasema uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki michuano hiyo utabakiwa kwa Zahera.

Alisema tayari ofisi yake imewasiliana na Zahera ukimjulisha kuhusu mwaliko huo.

 “ Tumepokea mwaliko kutoka Cecafa kuhusu Yanga kushiriki michuano ya Kagame, bado hatujafanya uamuzi kwa kuwa bado hatutajua ratiba za kocha, kama mnavyofahamu tumepata nafasi ya kushiriiki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa mantiki hiyo hata ratiba yetu itabadilika kutokana na ukubwa wa michuano hiyo.

“Tunajua ligi inaanza Agosti, Ligi ya Mabingwa Afrika nayo inaanza mwezi huo huo,  ukiangalia Kagame inaanza mwezi ujao, wakati huo bado michuano ya Afcon itakuwa inaendelea hivyo mipango yote ya maandalizi ya msimu na michuano yote anayo kocha, tutatarajia kupata jibu rasmi Jumatatu  kuhusu hatima yetu Kagame,”alisema  Katibu huyo mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).

Azam hadi sasa  ndio pekee kutoka Tanzania Bara iliyothibitisha kushiriki michuano hiyo huku ikiweka wazi kuwa itaanza maandalizi ya kutetea ubingwa wao Julai 20, ikiwa  chini ya kocha wao mpya, Etiene Ndayiragije.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles