25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

ZAFICO walia na ukosefu wa kiwanda cha dagaa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Licha ya zao la dagaa kupatikana kwa wingi visiwani Zanzibar, changamoto imetajwa kuwa ni ukosefu wa kiwanda cha kuhifadhi ili kuokoa zao hilo kupotea kutokana na umuhimu wake.

Akizungumza Julai 4, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 47 ya sabasaba, Mkuu wa Idara ya Fedha, Uwekezaji na Masoko wa Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO), Mwanaheri Mohamed Hilal amesema wanajishughulisha na mazao yote yanayopatikana baharini.

“Tumeanza na zao la dagaa na utafiti waliofanya tumeona lina fursa nyingi ndani na nje ya nchi, wahitaji ni wengi kila Mtanzania anauwezo wa kula zao hili hivyo tunarajia kujenga kiwanda Januari mwakani ambacho kitagharimu Sh bilioni 2.8 ili tuokoe dagaa wanaopotea kwani ndiyo imekuwa changamoto kubwa kwa sasaa,” amesema Mwanaheri.

Aidha, amesema wakijenga kiwanda hicho wafanyabiashara wa dagaa wataweza kutoa oda zao moja kwa moja kiwandani pia wataboresha mazingira ya wajasiriamali wa bidhaa hiyo.

Amesema wameanza kusanifu zao la dagaa na kuhakikisha wanaondoa changamoto zote zinazowakabili wajasiriamali wa zao hilo nakwamba malengo yao nikuwa na soko la dagaa ili TanTrade kuwaunganisha na soko huru la Afrika.

Mwanaheri amesema kwa sasa mikakati iliyopo ni kutosheleza soko la ndani kwani bado hawaja na masoko nje na kwamba wamepeleka sampuli ya bidhaa hiyo katika nchi za Uganda na Kenya.

“Changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni namna ya kuhifadhi bidhaa inapokuwa fresh inahitaji uangalizi wa hali ya juu kama hakuna uangalizi dagaa wataharibika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles