25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

YJ kutikisa Morogoro mkesha wa Christmas

NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa muziki nchini, Yakuti Joseph ‘YJ’ na kundi la Kanga Moko kutoka Dar es Salaam, wanatarajiwa kuwasha moto wa burudani katika shoo yake ya Vibe la XMass Eve & Mateka Tour itakyofanyika mkesha wa Christmas katika ukumbi wa Mahenge Hall.

Akizungumzia shoo hiyo babkubwa, YJ alisema onyesho hilo litafanyika pande za Kisaki ulipo ukumbi huo kuanzia usiku saa mbili hadi majogoo hiyo mashabiki wajiandae kupata burudani ya kutosha.

” Niliwamishi mashabiki zangu wa Morogoro, natarajia kuachia burudani ya kukata na shoka kutokana na ngoma zangu zote zilizotamba kama Achia niliyofanya na Ney wa Mitego na Stamina, Mdudu, Goma niliyofanya na Mzee wa Bwax, Nimevurugwa niliyomshirikisha Sholo Mwamba na nyingine kibao watu wasogee kwa kiingilio cha 5,000 tu na warembo wa Kanga Moko watakuwepo,” alisema YJ.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles